Kiisanzu

Kiisanzu (kinachojulikana pia kama Ihanzu au Nyisansu) ni lugha ya Kibantu inayeongelewa kwenye Bonde la Ufa la Tanzania.  Nilianza kusoma Kiisanzu mwaka 2016 na kazi yangu ya mwaka huu ni kuchanganua data zangu za lugha hii. Kinachofuata ni utangulizi wa Kiisanzu.

Isaac Isaac Shauri na Musa Gimbi wanaangalia mapicha ya ndege na kuyaelezana mmoja kwa mwingine. [Sehemu ya rekodi ya 20180704a (Harvey, forthcoming)]

Nchi ya kiasili ya Waisanzu huanza kwa mto Sibiti na kuendelea kusini kwa takriban kilometa 40. Kuanzia kilometa 20 inaanza kuingilia na nchi ya Wanyilamba. Vijiji vya wazungumzaji wa Kiisanzu zinaendelea magharibi mpaka mto wa Duromo (karibu ya ukuta moja kubwa wa Bonde la Ufa). Wazungumzaji hupatikana kwenye maeneo ya mashariki mpaka Haydom, wanapoishi pamoja na wazungumzaji wa Kiiraqw na lafudhi za Kidatooga. Mto Sibiti (ambayo maji yake huenda kaskazini) huingia kwenye ziwa Eyasi, na huko wazungumzaji wa Kiisanzu na Kihadza zinapakana.

Ramani inachoonyesha nchi ya kiasili ya Waisanzu.  Ziwa Eyasi ni kwenye eneo la kaskazini, na mto Sibiti hufuata njia inayefanana na mstari ya upande wa kushoto. Eneo la magharibi, mto Duromo huenda karibu ya ukuta kubwa wa Bonde la Ufa. Ramani kutoka Google Maps

Watafiti hawajahesabu idadi ya watu wanaoongea Kiisanzu, lakini kwenye kazi yake ya Atlasi ya Lugha za Tanzania, Mradi wa Lugha za Tanzania unakadiria kwamba, mwaka 2009, idadi ya wazungumzaji wa Kiisanzu ni 26,000 kwa ujumla.

Upisho wa Kiisanzu kutoka wazazi kwa watoto ni swali lingine ambaye jibu lake halijulikani vizuri. Mwaka 1987, mtafiti mmoja amekadiria kwamba idadi ya Waisanzu ilikuwa watu takriban 32,000, inayemaanisha kwamba namba ya 2009 inaonyesha upungufu wa wazungumzaji wa 20% kwenye maka 20. Nahisi kama kiwango hichi cha upotevu ni kubwa mno, hasa kwa sababu kuna watoto (hasa vijijini) waliojifunza na wanaozungumza lugha hii.

Hata hivyo, kuwapata wazungumzaji wa Kiisanzu kwenye mji kubwa wa karibu, Singida, ni vigumu, na watoto hawa wa familia ya Waisanzu hapa mjini hawatumii Kiisanzu sana, hata nyumbani.  Mara nyingi, wazungumzaji wa Kiisanzu wanasema kwamba lugha yao inamezwa na Kinyilamba: lugha kubwa inayepakana na Kiisanzu kwenye eneo ya kusini ya nchi ya Waisanzu. Utafiti zaidi huhitajikwa, lakini utaratibu huu huonyesha kwamba Kiisanzu ni lugha inayehatarishwa, hasa kwa lugha jirani yake, Kinyilamba.

Waisanzu wana hadithi nyingi kuhusu uhamishaji wa kihistoria kufika kwenye nchi yao ya sasa, mara nyingi Waisanzu wa kale wamehama kutoka kaskazini kwenda kusini, mara nyingi kupitia ziwa Nyanza (Victoria). Mapema, Waisanzu waliwashuku Wazungu wakoloni, na kwenye kipindi cha ukoloni, mara nyingi Waisanzu wamekuwa wanapinga.

Kwenye Bonde la Ufa la Tanzania, Waisanzu ni tofauti kwa sababu wako wakulima, na wanajiona hivyo (wakati makabila mengine huweza kuwa wakulima, lakini wanapenda zaidi kujitambua kama wafugaji). Mtama (na siku hizi, mahindi) ni mazao muhimu. Udugu hufuata upande wa mama na (hasa mapema kwenye ndoa), mume huishi kwa familia ya mke wake. Waisanzu wanafahamika sana kwenye Tanzania ya kati kama wataalamu wa kutengeneza mvua, taasisi inayeendelea mpaka sasa. Dini zipya (aina za Ukristo na Uislamu) hawajastawi sana hapa kama sehemu zingine, lakini Wakristo na Waislamu bado wapo, hasa kwenye miji na vijiji vikubwa. Dini zipya na imani ya kiasili huendelea pamoja.

Kiisanzu ni lugha ya Kibantu (kama vile Kizulu na Kiswahili). Kwa sababu ya ukosefu wa data, eneo lake la Kiisanzu kwenye familia ya Kibantu haijajulikana (k.m. kama Kiisanzu ni jamii ya lugha za “kikundi-F” kama Nyilamba, au kama Kiisanzu ni jamii ya kikundi tofauti ya lugha za Kibantu zilizokuwa Tanzania kabla ya mfiko wa lugha za “kikundi-F”). Kifonetiki, Kiisanzu kinakosa sauti za kikwamizwa za mdomo-meno (labio-dental fricatives) kama vile [f] na [v], na maneno mengi ambayo kwenye lugha za jirani yana sauti za [s] au [ʃ], kuna [h] (lingana mgosha ‘mwanamume’ kwenye Kinyilamba na mᵾgohá ‘mwanamume’) kwenye Kiisanzu. Kimofolojia, nomino zina kiambishiawali kinachotangulia kiambishiawali cha ngeli nomino (noun class prefix). Inaonekana kama kiambishiawali hiki hufanya kazi kama kibainishi bayana (definite article), lakini ni lazima data zaidi ziangaliwe kuhakikisha. Nomino za udogo huumbwa kwa kuongeza kiambishiawali ya ngwa- (lingana ngwana ‘mtoto’), kwa hiyo: ngwanyumba ‘nyumba ndogo, kinyumba’. Vitenzi jirejee (reciprocal and reflexive verbs) huumbwa kwa kiambishiawali -ki-, badala ya kiambishi tamati -an-. Kisintaksi, vishaji virejeshi (relative clauses) huumbwa kwa kiambishiawali n- badala ya kiambishi yambwa rejeshi (k.m. inyonyi nikimba ‘ndege anayeimba’). Ugunduzi zaidi utakuja na uchambuzi wingine.