Mihadhara

Harvey, Andrew. 2023. An Introduction to the Ihanzu Symposium 2023. Talk given at the Ihanzu Symposium 2023. Bielefeld University, Germany. 29.09.2023.

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Mkutano wa Ihanzu Symposium (yaani: mkutano wa Kigorowa) ni mfululizo wa mihadhara kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa kozi ‘Linguistic Field Research Methods’ (yaani: utafiti wa isimu wa maskanini) kushirika matokeo ya kazi yao kwa mzungumzaji mmoja wa lugha ya Kinyisanzu. Maoni haya hutoa taarifa ya ziada kuhusu lugha hii ya Kinyisanzu, kama vile sehemu inapoongelewa, umbile wa kozi, na ratiba ya mihadhara.
Angalia

Harvey, Andrew. 2023. An Introduction to the Gorwaa Symposium 2023. Talk given at the Gorwaa Symposium 2023. University of Bayreuth, Germany. 27.07.2023.

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Mkutano wa Gorwaa Symposium (yaani: mkutano wa Kigorowa) ni mfululizo wa mihadhara kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa kozi ‘Linguistic Field Research Methods’ (yaani: utafiti wa isimu wa maskanini) kushirika matokeo ya kazi yao kwa mzungumzaji mmoja wa lugha ya Kigorowa. Maoni haya hutoa taarifa ya ziada kuhusu lugha hii ya Kigorowa, kama vile sehemu inapoongelewa, umbile wa kozi, na ratiba ya mihadhara.
Angalia

Harvey, Andrew; Adoko, Daniel; Mensah, Samuel Obeng; Opoku, Enock Mensah; Opoku, Eunice; & Lartey, Samuel. 2023. Kinship Terms in the Tanzanian Rift: Initial Observations. Talk given at the Rift Valley Network Webinar Series. 26/07/2023. DOI: 10.5281/zenodo.8186829

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Bonde la Ufa la Tanzania ilionyeshwa kuwa na anuwai ya lugha pamoja na sehemu zinazofanana. Mhadhara huu ni jaribu la kwanza kupeleka uchambuzi huu kwenye maneno watu wanayotumia kwa ndugu wao. Wasilisho huu ni tokeo moja la kozi la Chuo Kikuu cha Bayreuth Language and Meaning (yaani: lugha na maana), sehemu yake moja ilikuwa kuhusu undugu na maneno ya kueleza undugu barani Afrika. Waliochangia kwenye kozi hii walichambua maneno ya undugu kutoka makala za anthropolojia na za isimu kuhusu jamii za Afrika, na walikusanya taarifa nyingi ya maneno (maneno ya undugu) na ya umbile (mifumo ya undugu). Wasilisho hutumia taarifa hii kama usuli wa kulinganisha lugha za Bonde la Ufa la Tanzania, kwa lengo la kuuliza maswali kuhusu vyanzo vya maneno na mifumo haya ya undugu, na kama zimerithiwa kijenetiki, kama zimeathiriwa na lugha zingine, au kama zilitengenezwa kuendana na mabadiliko makubwa zaidi ya jamii. Baada ya kuangalia undugu wa Bonde la Ufa la Tanzania kwa juu, wasilisho hutambulisha mifumo na hujaribu uchambuzi za mwanzo kwa kutumia uhusiano tatu wa undugu: 1) ndugu kama kaka na dada; 2) mipwa; na 3) kaka wa mama.
Angalia

Harvey, Andrew. 2023. Why do I gloss Gorwaa like that? Responses to an anonymous review of a rejected paper. Talk given at the Linguistics Colloquium. University of Bayreuth, Germany. 16.05.2023. DOI: 10.5281/zenodo.7883509

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Wasilisho huu hutolewa baada ya makala tarajiwa kukatazwa kwenye jarida la isimu Glossa. Makala kukatazwa sio ajabu – bali, ni kawaida sana – lakini maoni kadhaa wa mhakiki mmoja huchochea, husema kwamba uchambuzi wangu huchora lugha kama ya ajabu. Kwa sababu makala ilikatazwa, sijakuwa na nafasi rasmi kujibu maoni haya, ambayo siyakubali kabisa. Kwa sababu maoni haya yanahusika na ninavyoonyesha lugha ya Kigorowa, kuyajibu hunipa nafasi nzuri ya kufikiri kuhusu namna ninavyoeleza lugha hii, pamoja na kushiriki namna ninavyoelewa lugha hii ya Kigorowa.
Angalia

Harvey, Andrew. 2023. Introducing Gorwaa. Lecture given as part of the course “Linguistic Field Research Methods”. University of Bayreuth, Germany. 03.05.2023. DOI: 10.5281/zenodo.7855284

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Wasilisho la lugha ya Kigorowa, kutoka msingi wa kazi ya maskani na rekodi za sauti na video, kwa ajili ya kozi ya Chuo Kikuu cha Bayreuth ‘Linguistic Field Research Methods’ (yaani: utaratibu wa kiisimu wa maskanini).
Angalia

Harvey, Andrew. 2023. Retrospective of the Rift Valley Network Webinar Series Year 4. Talk given at the Rift Valley Network Webinar Series. 22/03/2023. DOI: 10.5281/zenodo.7762728

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Mhadhara huu hutazama mwaka wa tatu wa Rift Valley Network Webinar Series (yaani: mfululizo wa mihadhara mtandaoni wa Mtandao wa Bonde la Ufa), kwa lengo la kulinganisha na miaka yaliyopita, na kuangalia nyuzi zinazofanana kwenye utafiti wenu wa Bonde la Ufa, na kutambua nafasi kwa siku za mbeleni.
Angalia

Harvey, Andrew. 2022. Documenting Hadza 2019-2021: A retrospective. Talk given at the Research Colloquium for African Verbal and Visual Arts, University of Bayreuth. Bayreuth, Germany. 06/12/2022. DOI: 10.5281/zenodo.7393315

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Kutengeneza rekodi ya lugha ni uwanja muhimu wa sayansi ya isimu (yaani: linguistics) unayolenga utengenezaji wa rekodi ya kudumu ya lugha inachoweza kutumika na watu mbalimbali. Mhadhara huu hutazama mradi mmoja wa utafiti huu – mradi wa kutengeneza rekodi ya lugha ya Kihadzabe, iliyofadhiliwa na Endangered Languages Documentation Programme (ELDP) uliyotokea kati ya miaka 2019 na 2021. Baada ya kutoa taarifa za msingi, kuhusu lugha ya Kihadzabe na kuhusu watafiti wenyewe, mhadhara 1) hueleza mradi kwa kila hatua kama matayarisho, kazi ya kila siku, na kuweka kazi kwenye benki ya lugha; 2) huangalia matokeo kadhaa ya mradi, na 3) hutoa mawazo wa Wahadzabe waliohusishwa kwenye kazi hii.
Angalia

Harvey, Andrew. 2022. Gorwaa Selectors: A Verbal Analysis. Talk given at the Hybrid Workshop on Cushitic Languages, laboratoire Langage, Langues et Cultures D’Afrique (LLACAN), Centre National de la Recherche Scientifique (CNRS). Paris, France. 04/11/2022. DOI: 10.5281/zenodo.7258057

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Kikundi cha viangami kinachokaa kabla ya kitenzi (yaani: selector) ni muhimu sana kwenye sarufi ya Kigorowa, na lugha zingine za Kikushi cha Kusini (yaani: Southern Cushitic). Lakini picha yetu ya selector bado haijakamilishwa. Mhadhara huu huchambua selector ya Kigorowa kwa kuangalia mitindo yake ya mofolojia ni kisintaksi na huona kwamba selector ni kitenzi saidizi. Kwa kufanya uchambuzi huu mpya, mhadhara hutoa msingi kwa utafiti wa ndani zaidi wa mofosintaksi wa kitenzi cha Kigorowa.
Angalia

Harvey, Andrew. 2022. An Introduction to the Ihanzu Symposium. Talk given at the Ihanzu Symposium, Bielefeld University, Germany. 29/09/2022. DOI: 10.5281/zenodo.7180391

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Mkutano wa Ihanzu Symposium (yaani: mkutano wa Kinyisanzu) ni mfululizo wa mihadhara kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa kozi ‘Linguistic Field Methods’ (yaani: utafiti wa isimu wa maskanini) kushirika matokeo ya kazi yao kwa mzungumzaji mmoja wa lugha ya Kinyisanzu. Maona haya hutoa taarifa ya ziada kuhusu lugha hii ya Kinyisanzu, kama vile sehemu inapoongelewa, umbile wa kozi, na ratiba ya mihadhara.
Angalia

Harvey, Andrew. 2022. Learning from, Talking about, and Reflecting on Data Loss: A Failure Report. Talk given at the conference Where Do We Go From Here? Language Documentation and Archiving in the International Decade of Indigenous Languages. The Berlin-Brandenburg Academy of sciences and Humanities. Berlin, Germany. 07/10/2022. DOI: 10.5281/zenodo.7155475

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Griscom na Harvey (2020) ni rekodi kubwa yenye maada mbalimbali yanayohusika na lugha na asili za Wahadzabe wa Tanzania. Ilikusanywa kati ya miaka 2019 na 2021 kwa kuhusisha jamii, hata kama mkusanyiko huu ni mchango mkubwa kwa kazi ya lugha (linganisha Leonard 2021) kwa jamii ya Wahadzabe, sio kamili: wakati wa ukusanyaji wa rekodi za sauti na video, idadi kubwa ya video imepotezwa. Upotevu wa data hii itakuwa ini la mhadhara huu. Kurekodi na kueleza lugha ni kazi kubwa (linganisha Bowern 2008: 48), na changamoto – pamojawapo upotevu wa data (linganisha Tsutsui-Billins 2019) – huwa zinatokea. Hata hivyo, sio rahisi kwa wanaokusanya rekodi za lugha kuongea kuhusu changamoto zao – mwishoni hii kimya inasababisha changamoto hizi kutokea tena na tena. Mhadhara huu hupangwa kama ripoti ya changamoto (linganisha Engineers Without Borders Canada 2017) – changamoto huangaliwa kwa ndani, sababu za changamoto hutambuliwa, na mafundisho yake huorodheshwa. Mradi uliyozaa Griscom na Harvey (2020) ni, kwa namna nyingi sana, mfanikio kubwa sana, hasa kuhusu data zilizokusanywa, lakini pia kwenye mahusiano yaliyotengenezwa. Lakini kuongea kuhusu upotevu wa data uliyotokea ni muhimu kwa sababu kadhaa: inaweka wazi kilichotokea ili tunaweza kujifunza, inatengeneza eneo la kuongea kuhusu kazi ya jamii, na inatupa nafasi kuwaza kuhusu kazi yetu.
Angalia

Harvey, Andrew. 2022. More on Names and Naming in Gorwaa. Talk given at the 52nd Colloquium on African languages and Linguistics (CALL 2022). Leiden, the Netherlands 30/08/2022. DOI: 10.5281/zenodo.6990511

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Niliwahi kuongea kuhusu majina na utoaji wa majina kwenye Kigorowa, lakini data zile za zamani zilikuwa, kwa kiasi kubwa, kutoka Wagorowa wakieleza mfumo huu kwa jumla. Data mpya, hasa mahojiano pamoja na wazazi Wagorowa kuhusu watoto wao walivyopata majina yao, huongeza utondoti kwa ujuzi wetu, pamoja na data kuhusu Wagorowa wanavyofanya, zaidi ya wanavyosema kwamba wanavyofanya. Kwa kulenga maswali matatu – Majina ya Kigorowa hutolewaje?, Majini ya Kigorowa hutolewa na nani?, na Majina ya Kigorowa ni sanaa ya simulizi inayehatarishwa kwa kiasi gani na kwa namna gani? – mhadhara huu hutoa utondoti upya, upanusha uelewa wetu, na utukaribisha kwa picha ya kujuvya kwa sehemu hii muhimu ya lugha ya Kigorowa.
Angalia

Harvey, Andrew. 2022. Bantu Lexical Loans in Hadza: An introduction. Talk given at the 52nd Colloquium on African languages and Linguistics (CALL 2022). Leiden, the Netherlands 29/08/2022. DOI: 10.5281/zenodo.7016524

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Kihadzabe ni lugha tajiri ya maneno yaliyokopeshwa kutoka lugha tofautitofauti. Utafiti wa lugha ya Kihadzabe ni, kwa namna nyingi, bado kwenye utoto wake. Mhadhara huu hutoa wasilisho fupi kwa maneno yaliyokopeshwa kwenye Kihadzabe yanayofuatilika kwenye lugha za Kibantu, au yanayoonekana kuwa na asili za Kibantu.
Angalia

Harvey, Andrew. 2022. Deconstructing the “Hadza Curse”: Language work as work in transformation. Talk given at the evening lectures of the Leiden University Summer School in Languages and Linguistics. 28/07/2022. DOI: 10.5281/zenodo.6856975

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Kuna hekaya miongoni mwa wanaisimu inayosema kwamba anayejaribu kutafuta lugha ya Kihadzabe atashindwa. Kwa kuwa nimechochelewa na hadithi hii ya ajabu, mhadhara huu hutumia “Laana ya Kihadzabe” kama mlango kuangalia uhusiano kati ya watafiti na Wahadzabe, uhusiano kati ya utafiti unaohusika Wahadzabe na vurugu ya epistemiki, pamoja na uhusiano kati ya kazi ya lugha na kazi ya mgeuzo kuwezesha Wahadzabe kujithamini, kuongea, na kujiwakilisha wenyewe – zote kwa nia kihakiki. Mapema sana kwenye mhadhara huu, naweka imara kwamba “Laana ya Kihadzabe” imesababishwa na mambo nje ya madaraka ya Wahadzabe wenyewe, na ni jambo lililobuniwa tu. Uangalifu utabadilisha kutoka vitisho vilivyobuniwa dhidi ya wanaisimu kwa vitisho halisi dhidi ya Wahadzabe. Mhadhara huu unaweka imara kwamba kukomesha vurugu dhidi ya Wahadzabe ni lazima tubadilishe namna wanavyofafanuliwa kwa watu wa nje, hasa namna tunazofanya utafiti nao. Kazi ya hivi karibuni ya lugha na Wahadzabe inatolewa kama mfano wa mageuzo yanayotakiwa.
Angalia

Harvey, Andrew. 2022. The Ihanzu language and cultural material archive: an overview. Talk given at the Bielefeld University Linguistics Seminar Series. 13.07.2022. DOI: 10.5281/zenodo.6794044

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Harvey 2019 ni tokeo la kazi kubwa ya video na sauti iliyorekodi sehemu za lugha na utamaduni wa Wanyisanzu. Mhadhara huu 1) ni wasilisho la yaliyomo kwenye benki hii, 2) unatoa mafano ya namna benki hii inaweza kutafutwa, na 3) hutoa ‘uzi’ za benki hii zinazoweza kuwa muhimu kwa utafiti kwenye siku zitakazokuja.
Angalia

Andrason, Alexander, and Andrew Harvey. 2022. The form of emotions: The phonetics and morphology of interjections in Hadza. Talk given at the Rift Valley Network Webinar Series. 04.05.2022. DOI: 10.5281/zenodo.6518215

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Mhadhara huu hutoa uchambuzi wa kwanza wa maumbo (fonetiki na mofolojia) wa vihisishi vya Kihadzabe. Kwa kutumia utaratibu unaolenga mfano wa awali kwa jamii ya vihisishi, na kwa kutumia data mpya, wahadhiri wanaonyesha kwamba vihisishi vya Kihadzabe hufanana sana na mfano wa awali wa vihisishi. Vihisishi vya Kihadzabe vina sifa za mfano wa awali, na sifa zake zisizo za mfano wa awali zinafanana na zile zinazoonekana kwenye lugha tofautitofauti. Kwa kiasi kubwa, utafiti huu huthibitisha uhalali wa mfano wa awali unaelezwa kwenye masomo mengine, lakini utakaso kadhaa huongezwa pia.
Angalia

Harvey, Andrew. 2022. Retrospective of The Rift Valley Network Webinar Series – Year 3. Talk given at the Rift Valley Network Webinar Series. 23/03/2022. DOI: 10.5281/zenodo.6390804

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Mhadhara huu hutazama mwaka wa tatu wa Rift Valley Network Webinar Series (yaani: mfululizo wa mihadhara mtandaoni wa Mtandao wa Bonde la Ufa), kwa lengo la kulinganisha na miaka yaliyopita, na kuangalia nyuzi zinazofanana kwenye utafiti wenu wa Bonde la Ufa, na kutambua nafasi kwa siku za mbeleni.
Angalia

Harvey, Andrew. 2021. From construct state, to reference, and beyond: the linker morpheme in Gorwaa. Talk given as part of the This Time for Africa Lecture Series, Leiden University, Netherlands. 04.12.2021. DOI: 10.5281/zenodo.5757435

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Kiungo kwenye lugha ya Kigorowa ni mofimu ya kinomino chenye alomofu (yaani: umbo jingine la mofimu moja) sita tofauti kufuatana na jinsi. Mofimu kwenye herufi zito kwenye slufi wák “mdomo moja”, desir‘eé’ “msichana wangu”, hhawató baabá “mwanamume wa baba”; kurkí “mwaka huu”, ayeemá uren “nchi kubwa”, na /aylá tleer “wimbo wa harusi ndefu” zote ni viungo. Nomino hazionyeshi mofolojia ya kiungo kwenye mazingira haya: viima visivyo na vivumishi, yambwa zisizo na vivumishi kwenye ‘nafasi ya pili’ (yaani: kabla ya kundi la viangami linachokaa kabla ya kitenzi), na nomino zilizogubikwa. Nomino huonyesha viungo kwenye mazingira zote zingine. Makala mapema zaidi ya lugha za Kikushi cha Kusini hueleza viungo kama mofolojia ya construct state – muundo mmoja wa nomino kwenye lugha za Afroasiatiki zinapomilikiwa. Baadaye ya kuonyesha sababu umilikishaji hufai kueleza uwepo wa viungo vyote, wazo mbadala hutolewa: kwamba viungo vipo kwenye nomino zote zenye uhusianorejeshi, lakini hazitamkiwi zikikaa kwenye makali ya kulia ya kirai ya kifonolojia. Mwishoni, uchambuzi mpya kwenye Kerr (2020) huangaliwa, pamoja na njia kuelewa viungu vya Kigorowa vizuri zaidi.
Angalia

Mitchell, Alice, and Andrew Harvey. 2021. Riddles of the rift valley: a one-year update. Talk given at the Rift Valley Network Webinar Series. 01/12/2021. DOI: 10.5281/zenodo.5749215

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Wasilisho huu hutoa sasisho kuhusu kazi ya kushirikiana ya asili za mifumbo kwenye Bonde la Ufa, kazi ambaye wanachama wa RVN wameanza karibu mwaka mmoja uliyopita. Tunaonyesha malengo yetu na sababu ya kufanya kazi hii, pamoja na taarifa ya msingi kuhusu namna ambavyo kazi yetu ya kushirikiana kwa njia ya mtandao imwfanyika. Halafu tunatoa matokeo ya aina nne kutoka utafiti wetu wa mifumbo wa Bonde la Ufa: (i) mazingira ya mawasiliano; (ii) muundo wa mawasiliano; (iii) sarufi; na (iv) vipengele ya dhana na kimtindo.
Angalia

Harvey, Andrew. 2021. Remote but not distant: Lessons from fieldwork with Gorwaa, Hadza, and Ihanzu speaker communities. Talk given as part of the panel “Collaborative Linguistic Fieldwork During the Current Crises and Beyond” at the fourth School of Languages Conference (SOLCON IV), University of Ghana, Ghana (Online). 05.11.2021. DOI: 10.5281/zenodo.5647954

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Wasilisho uliyotolewa kama sehemu ya paneli la kuwa pamoja “Collaborative Linguistic Fieldwork During the Current Crises and Beyond” (yaani: kazi ya maskanini ya isimu wakati wa na mbali zaidi ya hali hii ya hatari) kwenye mkutano wa SOLCON IV.
Angalia

Harvey, Andrew. 2021. Developing New Africanists Symposium (Leiden 2021) – some opening remarks. Talk given at the Developing New Africanists Symposium. 18/10/2021.

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Mkutano wa Developing New Africanists (yaani: kuendeleza watafiti wa mambo ya Kiafrika) (DNA) ni mfululizo mfupi wa mawasilisho kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wa kozi ya Core Examples of Linguistic Structure (yaani: mifano mikuu ya umbile wa lugha) kukuuza kazi zao za lugha za Kigorowa, Kiiraqw, na Kihadzabe, pamoja na lugha za East Rift Southern Cushitic (yaani: Kikushi cha Kusini cha Bonde la Ufa la Mashariki), kuwa makala. Maoni haya huanzisha mkutano huu, pamoja na kutoa taarifa za ziada kuhusu lugha hizi.
Angalia

Gibson, Hannah, Andrew Harvey, and Richard Griscom. 2021. Preverbal clitic complexes in the Tanzanian Rift Valley Area. Talk given at the Rift Valley Network Webinar Series. 08/09/2021. DOI: 10.5281/zenodo.5497253

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Sura muhimu sana, Kießling et al. (2008), imetambua kwamba lugha nyingi za ente la Bonde la Ufa la Tanzania zina vikundi vya vitegemezi vyingi. Wametambua kwamba kuwa na vitegemezi kabla ya vitenzi sio kawaida kwenye ligha za Nilotiki wala lugha za Kibantu na kwa hiyo, hive vikundi via vitegemezi kabla ya kitenzi husababishwa na gusano ya lugha. Wasilisho hili hujenga kwenye msingi huu wa Kießling et al. (2008) na huangalia lugha zaidi, na huangalia data kwa ndani zaidi.
Angalia

Harvey, Andrew. 2021. Recalibrating documentation: reflections on 10 years of language documentation in the Tanzanian Rift. Talk given at the University of Bayreuth, Germany (Online). 22/06/2021. DOI: 10.5281/zenodo.4993449

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Hasa kuanzia karne hii mpya, kazi ya kurekodi lugha imebadilisha sayansi ya isimu, kwenye tunachoona kama data, pamoja na namna ambavyo data hii hukusanywa na hutumiwa. Wasilisho huu huangalia kazi yangu – miaka kumi ya kurekodi lugha kwenye eneo la Bonde la Ufa la Tanzania – kama mfano. Natafakari kuhusu namna ambavyo kazi yangu imebadilishwa. Naongea kuhusu kurekodi lugha kinachobadilisha namna ambavyo tunaeleza lugha, namna ambavyo tunagundua tamthali za semi mpya, na namna ambavyo tunasaidia jama ya lugha yenyewe. Mwishoni, wasilisho hutazama siku za mbele za kurekodi lugha barani Afrika, na mabadiliko yanayobaki kuhakikisha kwamba kazi hii ikae imara. Vile vile, zungumzo hili huangalia aina tofauti za ushikiamano, na kupinga kazi ya mtu mmoja tu. Mifano hutolewa kama rekodi na video kutokana na sanaa za semi za Wagorowa, Wanyisanzu, na Wahadza.
Angalia

Harvey, A. 2021. The lack of labiodentals in Ihanzu as a result of contact with Hadza. Talk given at the 10th World Congress of African Linguistics (WOCAL 10), Leiden University (Online). 10/06/2021. DOI: 10.17605/OSF.IO/HNDC5

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Lugha za Kibantu kwenye kikundi cha F31 Tanzania kaskazini-kati Kinyilamba na Kinyisanzu hazina sauti zinazotengenezwa na midomo kugusa meno (yaani: labiodentals). Hii hushangaza kwa sababu lugha zote zingine ndugu za Kinyilamba na Kinyisanzu — lugha za tawi la Takama — zote zina sauti hizi za labiodental. Kwa kuangalia lugha ya Kinyisanzu hasa hasa, wasilisho hili huonyesha kwamba ukosefu wa sauti za labiodental umesababishwa na kugusana na lugha kisiwa Kihadza. Baadaye ya kuongea kuhusu lugha ya Kinyisanzu na historia yake, wasilisho huangalia kazi ya Masele (2001) kuonyesha kwamba kila lugha ya Takama imezaa sauti za labiodental kwenye namna tofautitofauti kwa kubadilisha sauti au kuazima maneno, lakini Kinyisanzu hakijabadilisha sauti. Hali hii ya kuendeleza mitindo ya awali imesababishwa na mfumo unaofanana (yaani ukosefu wa sauti za labiodental) kwenye lugha ya Kihadza. Wasilisho hili huonyesha kwamba sauti ya [f] ni kitu kipya kwenye lugha ya Kihadza kutokana na kugusana na lugha ya Kikushi cha Kusini Kiiraqw. Wakati Kihadza na Kinyisanzu vimeanza kugusana, sauti ya [f] haijakuwepo kwenye Kihadza. Data zingine zisizohusika na lugha huangaliwa kuonyesha historia ya lugha hizi mbili, kama historia ya kuongea, hadithi za vyanzo vya jamii, na namna ya kufuata historia ya familia. Wasilisho hili huonyesha namna ambayo lugha isiyo ya Kibantu (Hadza) huweza kuathiri lugha ya Kibantu (Ihanzu) kwenye mazingira makubwa zaidi yenye lugha nyingi sana ya eneo la Bonde la Ufa la Tanzania.
Angalia

Griscom, Richard, Andrew Harvey, Alain Ghio, and Didier Demolin. 2021. Distinctive features and articulatory gestures in Hadza. Talk given at the 10th World Congress of African Linguistics (WOCAL 10), Leiden University (Online). 10/06/2021. DOI: 10.17605/OSF.IO/Q8PSX

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Lugha ya Kihadza ina sauti za vidoko kadhaa. Sands, Maddieson & Ladefoged (1996) na Sands (2013) hueleza sauti za vidoko 9 kwenye Kihadza, wakati Miller (2008) husema kwamba ziko 12. Aina nne za sauti za vidoko za Kihadza [ʘ, |, !, ‖] bilabial, dental, alveolar na lateral huweza kutamka (kwenye namna ya kuzitofautisha) kwenye namna ya aspiartion, glottal, na nasali [ʘ̰ , | ʔ, | h, ŋ|, ŋ| ʔ, ! ʔ, ! h, ŋ!, ŋ! ʔ, ‖, ‖ h, ŋ‖ h, ŋ‖ ʔ]. Tukianagalia sauti zio, vidoko vya Kihadza huweza kueleza kama [grave] vs. [acute] na [abrupt] vs. [noisy], kutokana na Traill (1994). Kueleza vidoko vya Kihadza kama vitendo (vilivyotendeka kwa muda) na kuelewa kinachozitofautisha, wanawake wanne na wanaume watano wanaoweza kuongea Kihadza walirekodiwa kwa kutumia mashine mbalimbali (Aerodynamic, acoustic, EGG, palatografia na video). Matokeo kadhaa huonyesha kwamba kuna tofauti kati ya vidoko vya ncha ya ulimi [|, !] na ile iliyotengenezwa na upande wa ulimi [‖]. Mwendo wa ulimi ni taratibu zaidi kwenye vidoko vya [+aspirated] julio vidoko vea [-aspirated].
Angalia

Coburn, J., Sands, B., Harvey, A., and Griscom, R. 2021. Tonal patterns of Hadza nouns. Talk given at the 10th World Congress of African Linguistics (WOCAL 10), Leiden University (Online). 07/06/2021. DOI: 10.17605/OSF.IO/8PY5U

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Kwenye washilisho hili tunaonyesha chambuzi mpya la toni ya Kihadza. Kwenye kazi ya awali, toni imeelezwa kama mali ya silabi (Sands 2013, Tucker et al. 1977), lakini sisi tunaonyesha kwamba kinachobeba toni ni mora. Kutokana na data zilizokusanywa mwaka 2019 na 2020 kutoka eneo nne ambazo Hadza huongelewa, tunaonyesha kwamba mamora zinaweza kuwa na toni ya H au la (ambazo hutokea kama toni ya chini). Zaidi ya kuonyesha taipolojia ya mitindo ya toni kwenye mizizi ya Kihadza, tunaonyesha taipolojia ya mitindo ya ukubwa. Namna ambazo mfumo ya prosodia na toni huingiliana itaongelewa. Kwa mfano, kiambishi cha 3sg.f /-ko/ huonyesha toni ya juu kwenye sentensi kama (‘niliona X kule’), au kwenye orodha (wakati kumaanisha kwamba sentensi huendelea); lakini ikitokea mwisho wa sentensi /-ko/ huweza kuwa na toni ya chini. Kinachovutia, hata kama Kihadza kina sauti za konsonanti nyingi, Kihadza hakina sheria zinazokataa konsonanti fulani na toni fulani kutokea pamoja.
Angalia

Harvey, Andrew. 2021. Introducing Ihanzu: contexts, basics, and puzzles. Lecture given as part of the course “Introduction to Field Methods”. Bielefeld University, Germany. 28/05/2021. DOI: 10.5281/zenodo.4890358

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Rudio la lugha ya Kinyisanzu, kutokana na kazi ya maskanini na rekodi za lugha. Kwa ajili ya kozi ya Chuo Kikuu cha Bielefeld “Introduction to Field Methods”.
Angalia

Harvey, Andrew and Richard Griscom. 2021. Can the Subaltern Document? A mixed methods analysis of community-led language documentation. Talk given at the Leiden University Centre for Linguistics Sociolinguistics Seminar Series. 14/05/2021. DOI: 10.5281/zenodo.4757576

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Wakati wa kuhusisha watu wa jamiilugha kwenye kazi ya kurekodi lugha yao, ni kawaida kuchagua wazungumzaji waliosoma shuleni au wanaojua teknolojia mbalimbali. Je, kuna utaratibu gani kufanya kazi kwenye majamiilugha yanayokosa zote mbili? Wasilisho hili hueleza kazi za zaidi ya miaka kumi zinaohusisha majamiilugha manne tofauti kwa Bonde la Ufa la Tanzania – yote yanayokaa nje ya mfumo wa nguvu wa kisiasa. Tunajaribu hapa kuonyesha kwamba utafiti kwenye mazingira haya unaohusisha watu wa jamiilugha huwezekana, na zaidi ya hii, huleta matokeo mazuri zaidi. Kwa namna za uchambuaji mbalimbali tunaonyesha kwamba utafiti unaoongozwa na watu wa jamiilugha hutengeneza rekodi za lugha pana zaidi kuliko zile zilizotengenezwa na watafiti wasio wa jamiilugha. Pamoja na hii tunaeleza kwamba, hasa kwa watu kutoka jamii nje ya mfumo wa nguvu wa kisiasa, mtafiti unaoongozwa na watu wa jamiilugha hutengeneza rekodi zenye thamani kubwa zaidi kwa jamiilugha lenyewe. Miongoni mwa uchambuaji wetu, tunalinganisha mtindo wa kazi wa watu wasio wa jamiilugha na mitindo ya kazi za watu wa jamiilugha, na tunaangalia tofauti zilizopo.
Angalia

Harvey, Andrew and Richard Griscom. 2021. Retrospective of the Rift Valley Network Webinar Series, Year 2. Talk given at the Rift Valley Network Webinar Series. Online. 24/03/2021. DOI: 10.5281/zenodo.4636828

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Mhadhara huu huangalia mwaka wa kwanza wa Rift Valley Network Webinar Series, kutambua maada yanayozungumziwa sana pamoja na nafasi ya maendeleo za siku zijazo.
Angalia

Griscom, Richard, and Andrew Harvey. 2021. Community members make a more comprehensive documentary record. Talk given at the 7th International Conference on Language Documentation and Conservation (ICLDC). Online. 04/02/2021. DOI: 10.5281/zenodo.4621164

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Maandiko kuhusu utengenezaji wa rekodi ya lugha huongea kuhusu umuhimu wa kutengeneza mahusiano na jamiilugha na huhamasisha ushirikiano wa jamiilugha (Arka 2018, de Lima Silva na Riestenberg 2020, Vallejos 2014). Lakini mpaka sasa, vitu vilivorekodiwa na watu kutoka nje ya jamiilugha na watu wa jamiilugha havijawahi kulinganishwa. Wasilisho hili huangalia vipengele viwili vinavyothaminiwa kwenye kazi ya kurekodi lugha, na huangalia rekodi zilizofanywa na watafiti kutoka nje ya jamiilugha na watu wa jamiilugha. Jamiilugha husika ni akina Kiasimjeeg Datooga (Griscom 2018), Kigorowa (Harvey 2017), Kihadza (Griscom and Harvey 2020), na Kinyisanzu (Harvey 2019).
Angalia

Harvey, Andrew, and Chrispina Alphonce. 2021. Names and Naming in Gorwaa and Iraqw: a typological Tanzanian perspective. Talk given at the American Name Society Annual Meeting 2021, Online. 24/01/2021. DOI: 10.5281/zenodo.4454874

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Lugha za Kikushi cha Kusini Kigorwaa (ISO639-3: gow) na Kiiraqw (ISO639-3: irk) – zinazozungumzwa nchini Tanzania kwa watu 130,000 na 500,000 – ziko kati ya idadi ndogo ya lugha za Kikushi za nchi hii, na hutofautishana kwa fonolojia, sarufi, na utamaduni wa jamiilugha zao. Wanaisimu kutoka nje ya jamiilugha (Harvey 2019) na ndani ya jamiilugha (Alphonce 2020) huonyesha kwamba utoaji wa majina wa Wagorwaa na Wairaqw ni muhimu kuendeleza historia, na zinahatarishwa kwa mifumo ya utoaji wa majina ya Kikristo, Kiislamu, na Kiswahili. Kazi hizi zilizotajwa juu hujaribu kuchambua majina na utoaji wa majina kwa Wagorwaa na Wairaqw, lakini haziweki mifumo haya kwenye mazingira yake ya mifumo tofauti nchini Tanzania. Washilisho hili huanza kwa maelezo kuhusu mifumo ya Kigorwaa na Kiiraqw, kama majina ya kurithi, majina yanayoeleza mazingira mtoto alizaliwapo, na majina yanayoepusha kifo. Halafu, kwa kuangalia uchambuzi wengine kutoka jamiilugha zingine, mifumo ya Kigorowa na Kiiraqw hulinganishwa na hutofautishwa na mifumo ya jamiilugha za Kibantu-, Kiniloti, na Kihadza.
Angalia

Harvey, Andrew. 2020. Riddles in Ihanzu. Talk given at the Rift Valley Network Workshop “Riddles of the Rift Valley: Variation and convergence in a verbal genre”. 20/11/2020. DOI: 10.5281/zenodo.4294076

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Muhtasari wa vitendawili na utoaji wa vitendawili wa Kinyisanzu.
Angalia

Harvey, Andrew, and Richard Griscom. 2020. Who are the Hadza? A linguistic perspective. Talk given at CALL 50, Leiden University. 31/08/2020. DOI: 10.5281/zenodo.4021116

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Mhadhara huu hutoa maelezo kutoka kazi yetu ya kurekodi lugha, hasa kuhusu Kihadza huongelewa wapi, huongelewa na nani, na namna hutumiwa. Kwa sababu ya aina ya maswali tunayojaribu kujibu (ambayo ni kuhusu anayoongea Kihadza, na sio nani anayotambuliwa kama Mhadza), picha ya Wahadza kutoka kazi yetu ni tofauti sana kuliko zile zilizotokea zamani. Tunaonyesha mifano ya Kihadza na namna kinavyotumika kwenye mazingira yake, na tunalinganisha mifano hii na maelezo ya zamani. Lengo moja ya mhadhara huu linahusika isimu: kuonyesha data mpya kutoka jamii ya lugha isiotafutwa sana. Lengo lingine ni kuangalia utafiti wa zamani uliopuuza kiasi kikubwa cha Wahadzabe.
Angalia

Harvey, Andrew. 2020. The Gorwaa symposium: some opening remarks. Talk given at the Gorwaa Symposium, Leiden University, the Netherlands. 27/08/2020. DOI: 10.5281/zenodo.4004902

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Kikao cha Kigorowa (yaani: The Gorwaa Symposium) ni kikundi cha mihadhara kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi kutoka ‘Core Examples of Linguistic Structure’ kubadilisha kazi yao kuwa makala. Maneno haya ni kuchora picha ya Kigorowa: huongelewa wapi, mfano wa rekodi yake, na maswali yasiyojibika mpaka sasa.
Angalia

Harvey, Andrew. 2020. Verbal paradigms in Gorwaa: phonological analysis in service of a unified account. Talk given at the Rift Valley Network Webinar Series. 06/05/2020. DOI: 10.5281/zenodo.3816950

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Kwa kawaida, vitenzi vya Kigorowa huwekwa kwenye vikundi sita vya uambishaji. Mhadhara huu ni uchambuzi wa kifonetiki kwa vitenzi vya Kigorowa, na huangalia mabadiliko ya kifonetiki (sonorization/desonorization) kupunguza idadi ya vikundi vya uambishaji.
Angalia

Harvey, Andrew and Richard Griscom. 2020. Retrospective of the RVN Webinar Series, Year One. Talk given at the Rift Valley Network Webinar Series. 25/03/2020. DOI: 10.5281/zenodo.3730625

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Mhadhara huu huangalia mwaka wa kwanza wa Rift Valley Network Webinar Series, kutambua maada yanayozungumziwa sana pamoja na nafasi ya maendeleo za siku zijazo.
Angalia

Harvey, Andrew, and Daisuke Shinagawa. 2020. Tone in Ihanzu. Talk given at the Rift Valley Webinar Series 11/03/2020. DOI: 10.5281/zenodo.3707591

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Lugha ya Kinyisanzu ina toni mbili tofauti: chini (sifuri) na juu. Mhadhara huu, unaotumia rekodi za sauti mpya kutoka utafiti upya wa Kinyisanzu, huangalia aina za masharti yanayoendesha matamshi ya toni kwenye lugha hii.
Angalia

Harvey, Andrew. 2019. Language documentation: a view from the Tanzanian Rift Valley. Talk given at the African Studies Association of Africa conference, Nairobi, Kenya. 25/10/2019. DOI: 10.5281/zenodo.3526878

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Kazi ya kurekodi lugha (yaani: language documentation) (hasa kama ilivyoelezwa kwenye Himmelmann 1998) hubadilika sana barani Afrika (linganisha Seyfeddinipur (ed.) 2016). Kwa kuangalia Eneo la Bonde la Ufa la Tanzania (kama walivyoongea Kießling, Mous, na Nurse 2008), mhadhara huu huangalia namna kazi ya kurekodi lugha barani Afrika 1) ni imara zaidi inapoelewa asili ya uigizaji (yaani: performativeness) kwenye ini wa kuwasiliana; 2) hushindwa inapojaribu kutii ratiba za kuweka lugha kwenye kiandiko, na 3) huonyesha nafasi kubwa sana kwa kufanya kazi kufuata asili za lugha kama mtindo wa kuongea (c.f. Ameka 2015).
Angalia

Harvey, Andrew. 2019. Names and naming in Gorwaa. Talk given at the African Studies Association of Africa conference, Nairobi, Kenya. 24/10/2019. DOI: 10.5281/zenodo.3523431

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Kigorowa (South Cushitic, Afro-Asiatic) ni lugha inayehatarishwa, na huzungumzwa na watu takriban 133,000 kwenye wilaya za Babati, Tanzania kati. Utafiti kuhusu matumizi ya majina ya kiasili ya Kigorowa huonyesha kwamba watu hawayatumia sana kama zamani, na siku hizi hufadhali majina ya Kikristo, Kiislamu na Kiswahili. Kwa hiyo, hata hii asili ya kutoa majina limehatarishwa. Hii ni muhimu, kwa sababu majina ya watu na namna yanavyopewa watu hutupa namna mmoja kujifunza kuhusu utamaduni wa watu, pamoja na historia ya lugha yenyewe. Kwa njia za kuongea na watu, kusikiliza historia za maisha kwenye Gorwaa language and cultural material archive, na kwa kutumia orodha ya majina 750 ya Kigorowa niliyekusanya wakati wa utafiti wangu Babati kati ya miaka 2012 na 2016, natoa maelezo kuhusu mtindo wa utoaji wa majina miongoni mwa Wagorowa. Majina mengi hutoka nomino za Kigorowa na zinahusu vitendo au matukio – mtindo kawaida sana barani Afrika. Majina mengi hufanya kazi kulinda dhidi ya ubaya, kuhakikisha historia ya familia, na kuwasifu watu wenye nguvu. Makopesho kutoka lugha za Kidatooga ni namna moja kuona migusano kati ya watu Wagorowa na Wadatooga kwenye Eneo la Bonde la Ufa. Makopesho ya siku hizi kutoka Kiswahili na Kiingereza hutufundisha kuhusu migusano hii za kisasa.
Angalia

Harvey, Andrew, and Richard Griscom. 2019. Hadza: A century of research. Talk given at the African Studies Association of Africa conference, Nairobi, Kenya. 24/10/2019. DOI: 10.5281/zenodo.3514345

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Wawindaji-wakusanyaji wanaozungumza lugha ya vidoko, Wahadzabe ni watu wanaovutia sana kwenye Eneo la Bondo la Ufa la Tanzania, na wamekuwa shahaba la watafitu nchini Tanzania kwa zaidi ya miaka mia moja. Kwa kuangalia masomo ya isimu na anthropolojia, mhadhara huu hufuata zungumzo la watafiti kuhusu Wahadzabe, na hasa, namna zungumzo hili limeathiri namna tunavyoelewa Wahadzabe leo. Wazo lenye nguvu ni kuona Wahadza kama watu waliokaa mbali kwa makundi mengine, na wasiobadilika sana kwenye miaka mingi. Tunachoonyesha ni namna wazo hili lilivyoingia kwenye akili za watu wa nje, na namna lilivyoathiri watu Wahadza leo. Halafu, tunaonyesha namna wanaisimu wameanza kuangalia wazo hili, na kulibadilisha.
Angalia

Harvey, Andrew. 2019. Nonconfigurationality in Gorwaa. Talk given at the Rift Valley Network Webinar Series. 07/08/2019. DOI: 10.5281/zenodo.3361213

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Utafiti upya huonyesha kwamba Kigorowa (Kikushi cha kusini, Tanzania) ni lugha lenye umbo huru (yaani: non-configurational language). Viwakilishi huweza kuachwa (yaani: radical pro-drop), mpangilio wa maneno ni huru (yaani: word order is free) , na viambajengo katizwa (yaani: discontinuous constituents) vinapatikana. Mhadhara huu huonyesha mambo haya, na huangalia mawazo mawili kuhusu muundo virai (yaani: phrase structure) huu (wazo la Pronominal Argument (Jelinek (1984), Baker (1996)), na wazo la Mirror Theory (Adger, Harbour, na Watkins 2009). Mambo yatayoangaliwa ni aina mbalimbali za mitindo ya mofosintaksi, ambazo kadhaa hazijawahi kuangaliwa kwenye lugha za Kikushi cha kusini.
Angalia

Harvey, Andrew. 2019. Preverbal particles in Ihanzu. Talk given at Workshop on Bantu in contact with non-Bantu, ILCAA, TUFS. 27/06/2019. DOI: 10.5281/zenodo.3250524

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Eneo la Bonde la Ufa la Tanzania, kama walivyotambua Kießling, Mous, na Nurse (2008) ni sehemu muhimu barani Afrika kwa sababu ni eneo pekee ambapo familia za lugha kubwa nne zote huongelewa na hugusana kwa muda mrefu (Afro-asiatic, Khoisan, Niger-Congo, na Nilo-Saharan). Kwenye kazi hii hii, wametambua mambo ya kuangaliwa 19 (kifonolojia, kimofosintaksi, na chamali) zinazopatikana kwenye familia zaidi ya moja, na ambazo zinaweza kusababishwa na migusano kati ya lugha hizi. Kwenye mambo haya 19, moja muhimu sana ni kundi la viangami kabla ya kitenzi (yaani: preverbal clitic complex): mfululizo wa faridipeke chamilifu (yaani: a series of functional particles) zinazofanya kazi ambazo kitenzi kinazofanya kwenye lugha zingine. Mhadhara huu huangalia faridipeke chamilifu zinazotangulia kitenzi kwenye lugha ya Kinyisanzu. Kutoka utafiti upya, mhadhara huu huongeza uelewa wetu wa Kinyisanzu – lugha yenye utafiti uchache inayekaa kandokando ya Eneo la Bonde la Ufa la Kitanzania – na unarudi kwenye historia ya migusano ya lugha inayehadithia kwa njia ya faridipeke hizi.
Angalia

Griscom, Richard, Andrew Harvey, and Jeremy Coburn. 2019. Rift Valley bibliography: an introduction. Talk given at the Rift Valley Network Webinar Series. 10/07/2019. DOI: 10.5281/zenodo.3270592

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
The Rift Valley Bibliography ni mkusanyo wa viambatisho vinavyohusika na Eneo la Bonde la Ufa Tanzania (Kießling et al. 2008). Toleo 1.0 ya Bibliography ina viambatisho zaidi ya 400, pamoja na faili za PDF zinazopatikana bure kwa wanaojiunga kwa Rift Valley Network. Wakati wa kuonyesha Bibliography hii, tunaeleza yaliyomo, namna unavyoweza kutumika, na njia wanaojiunga kwa Rift Valley Network waweze kusaidia kutengeneza toleo zipya.
Angalia

Harvey, Andrew. 2019. The Gorwaa language and cultural material archive: an overview. Talk given at the Rift Valley Network Webinar Series. 29/05/2019. DOI: 10.5281/zenodo.3052679

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Harvey 2017 ni tokeo la ukusanyaji wa data zinazohusika na lugha na asili ya Wagorowa. Hotuba hii 1) huonyesha maada yaliomo ndani ya akiba hii, 2) hutoa mifano ya namna za kutumia akiba hii, na 3) hueleza mawazo kadhaa kuhusu vitu ambavyo huweza kutafutwa kwa kutumia akiba.
Angalia

Griscom, Richard, and Andrew Harvey. 2019. The Tanzanian Rift Valley Area: a prolegomenon for research and a network. Talk given at the Rift Valley Network Webinar Series. 20/03/2019. DOI: 10.5281/zenodo.2595908

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Eneo la Bonde la Ufa la Tanzania ni pekee barani Afrika kwa sababu familia za lugha za Kiafrika zote kubwa zimepakana hapa kwa muda mrefu (lingana Kießling, Mous, na Nurse 2008, ambaye huitwa KMN 2008 hapo chini). KMN 2008, andiko muhimu sana kwa masomo ya Bonde la Ufa kama eneo la lugha, husema kwamba lugha zinazohusika ni: Kiiraqw, Kigorowa, Chasi, Kiburunge, (zote Lugha za Kikushi cha Kusini), Kinyaturu, Kirangi, Kimbugwe, Kinyilamba, Kinyisanzu, Kikimbu (lugha za Kibantu); Kisandawe (Kikhoisan); Kidatooga (Kinailoti cha Kusini), pamoja na Kihadza (ambaye haipo kwenye familia kubwa zaidi). Pia, ni muhimu kusema kwamba Datooga ni kundi la lafudhi zinazotafautiana. Pamoja na hii, lugha zinazoitwa “Dorobo” pamoja na vile vile lugha zilizopotezwa Aasax na Kw’adza (Kikushi cha Kusini) ziko kwenye hili kundi la lugha za Bonde la Ufa pia. Kwenye hotuba hii, 1) tunazungumza kuhusu eneo letu, jiografia na mazingira yake, watu wanaozungumza lugha hizi, pamoja na utafiti uliotangulia na kuchambua historia, asili, na lugha za watu hawa, 2) tunazungumza kuhusu hitaji la Mtandao wa Watafiti wa Bonde la Ufa sasa, na kufafanua watu kwenye mtandao wetu mpaka sasa, pamoja na kazi yao.
Angalia

Harvey, Andrew. 2019. Ihanzu: an initial profile of a Bantu language of the Tanzanian Rift Valley. Talk given at Workshop on the Description and Analysis of Tanzanian Languages, ILCAA, TUFS. 23/01/2019. DOI: 10.5281/zenodo.2532173

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Kiihanzu ni lugha ya Kibantu ya Bonde la Ufa la Tanzania, inayefahamika vidogo sana na wanaisimu. Kwa sababu hakuna kitabu cha sarufi, kamusi, au vitabu vya hadithi, lugha hii haijaelezwa hata kidogo. Kwa kutumia data zilizokusanywa miaka 2016 na 2018, hotuba hii inatoa ripoti ya mwanzo ya lugha ya Kiisanzu: mazingira yake (k.m. wapi huongelewa, na kwa nani, hali yake ya kufundishwa kwa watoto, n.k.), pamoja na chanzo chake na hali yake ya kihistoria kwenye eneo la Bonde la Ufa. Pia, hotuba hutoa maelezo kuhusu sarufi yake (fonolojia, mofolojia, pamoja na sintaksi). Hotuba humaliza kwa kutoa taarifa kuhusu hatua za utafiti zitakazofuata hivi punde, pamoja na manufaa ya siku za mbele kutoka kazi ya kusoma, kueleza, na kutunga kumbukumbu ya lugha hii.
Angalia

Harvey, Andrew. 2018. Beyond the trilogy: a vision for expanded Boasian documentary outcomes. Talk given at LingDy Forum, ILCAA, TUFS.19/12/2018. DOI: 10.5281/zenodo.2380217

Tambua kwamba: Hotuba hii haijapitishwa kwa wataalam wengine. Kwa hiyo, matokeo yake ni ya kujaribia tu, na huweza kubadilisha.

Muhtasari
Miaka kumi baadaye ya utoaji wa ‘Essentials of Language Documentation’ ya Gippert, Himmelmann, na Mosel (2008), udhaifu nyingi walizoona kwenye matokeo ya uelezaji wa lugha (language description) zinabaki. Hotuba hii inahusu udhaifu mbili walizozungumza zinazohusika na fungu la Kiboas (Boasian trilogy), yaani, kwamba i) “ukitumia kitabu cha sarufi na kamusi ya lugha fulani, namna lugha hii inavyoongelewa bado havijulikani [k.m.] utaratibu wa mazungumzo ya kila siku zikoje […] au namna watu huwasiliana wakati wa kujenga nyumba au kujadiliana mahari”, na ii) “vitabu vya sarufi na kamusi huleta maada machache sana yanayeweza kutumika kwa watu wasio wanaisimu [hasa, kwa ajili ya hotuba hii] watafiti wa masomo mengine (k.m. wanahistoria, wanaanthropolojia, n.k.) (k.19). Baadaye ya ukaguzi wa fungu la Kiboas na tatizo la kuingiza kila jinsi la lugha ndani lake, hotuba hii huangalia matokeo ya uelezaji wa lugha tofauti, kama vile sarufi za matumizi ya lugha (grammars of language use), mikusanyiko ya viziada lugha (paralinguistic repertoires), ethnolojia za taratibu za mawasiliano (ethnographies of communication), na tezauri za kiethnolojia (ethno-thesauruses). Hotuba hufunga kwa kurudi kwenye dhana ya ‘maandiko’ (texts) kama kiunganisho cha matokeo haya yote, na kwa kuongea kuhusu vinyume vya maoni hii ya fungu la kiboas lililopanuliwa kwenye kazi ya kutengeneza kumbukumu la lugha (language documentation).
Angalia